
MASIKINI wa
Mungu mama huyu wa kijiji cha Buhundwe wilayani Rorya mkoani Mara
akitambulika kwa jina la Catherine Benedicto, amepokea kichapo kikali
toka kwa mwanamke mwenzie aliyetajwa kwa jina la Bi. Tatu Wambura kwa
kosa la eti kupitisha ng'ombe kwenye eneo la shamba linalomilikiwa na
Bi. Tatu.
Inatajwa kuwa jumatano katikati ya
wiki tunayoimalizia majira ya saa sita mchana, Catherine akiwa anaswaga
ng'ombe wake wapatao 30 hivi na ushee kutoka nyumbani kwake kuelekea
malishoni alipitisha mifugo hiyo katika shamba la Bi Tatu Wambura,
ambalo hata hivyo lilikuwa halijalimwa wala halikuwa na mazao yoyote na
ndipo alipoonwa na Bi Tatu alivamiwa na kupewa kipigo kikali
kilichoambatana na makofi na mangumi hata kumpelekea mwanamama huyo
kupata maumivu makali sambamba na uvimbeckatika baadhi ya sehemu zake za
mwili hasa jichoni.

Hadi
kamera yetu inaondoka eneo la tukio suala hilo lilikuwa tayari
limefikishwa mbele ya uongozi wa kijiji na tayari hatua za kisheria
zilikuwa zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni sambamba na taratibu za matibabu
kwa Bi. Catherine.
Tukio hili linatokea ikiwa ni siku
chache tu taifa la Tanzania likitoka kuungana na nchi nyingine
ulimwenguni kuadhimisha siku ya Mwanamke duniani ambapo suala la
unyanyasaji na ukatili limekuwa likitizamwa na kukemewa huku mtu ambaye
anatajwa sana kuhusishwa na ukandamizaji pamoja na ufanyaji ukatili
akitajwa kuwa ni mwanamme.
Lakini kwa taswira hii ya mwanamke kumpiga mwanamke mwenzie tena kwa kumshambulia kiasi cha kutisha inaleta taswira gani?

Ni moja kati ya
baadhi ya nyumba majirani za watu wa kijiji cha Buhundwe wilayani Rorya
mkoani Mara, maisha yanaendelea na hapa binti mdogo Robi akitimiza
majukumu ya nyumbani kama mtoto.
PICHA NA ZEPHANIA MANDIA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment