April 22, 2014

 

 Binti Fauzia akiwa amepozi nyumbani kwao maeneo ya Kigogo jijini Dar es Salaam

NI lipi hujasikia? Linaweza kuwa hili! Binti mmoja aliyetambulishwa kwa jina la  Fauzia (jina la mbele lipo), mwenye umri wa miaka 16, mkazi wa Kigogo jijini Dar amedai kutumikia nafasi ya umalkia katika imani yenye utata duniani ya Freemason, Uwazi linakudondoshea.
Binti huyo alikwenda mbele zaidi kwa kudai kwamba ili kujiunga na imani hiyo, alimuua mama yake mdogo kwa ajili ya kafara.
Akizungumza na gazeti hili siku chache baada ya kuokoka akiwa nyumbani kwa baba yake mdogo, Kigogo, Fauzia alisema alitokea Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alipokuwa akiishi na bibi yake. 

Alikuja Dar kwa lengo la kuendeleza mauaji ya kafara ambapo safari hii ilikuwa amuue mama yake mdogo mwingine ambaye ni mjamzito kwa sasa. 
Alisema kama angefanikiwa kumuua, angepandishwa cheo na kuwa malkia kamili katika jamii hiyo inayotafsiriwa vibaya duniani.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE