April 13, 2014

Mawasiliano ya barabara kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo yamejifunga kutokana na barabara hiyo kubomolewa na maji katika Daraja la Mpiji mpakani mwa mikoa wa Dar es Salaam na Pwani.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alifanikiwa kufika katika eneo hilo mara tu baada ya kupokea taarifa za kukatika kwa barabara hiyo. Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe pamoja na watendaji wengine kutoka TANROADS, Waziri Magufuli amewaagiza watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafanyakazi mchana na usiku ili barabara hiyo muhimu na yeye kupitisha magari mengi ifunguliwe mapema iwezekanavyo.

Zaidi ya maelekezo hayo, Mhe. Magufuli pia ameagiza kuahirishwa hadi itakapopangwa baadaye kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kuanzia siku ya Jumanne ya tarehe 15 Aprili 2014 huko mkoani Tanga. Hatua hiyo imechukuliwa ili watendaji hao wabaki katika vituo vyao vya kazi hadi hali ya mvua zinazoendelea kutulia na taarifa nyingine kutolewa.

Akizungumzia hali katika eneo hilo la Mpiji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe kwa upande mwingine alibainisha kuwa kilichozolewa na maji ni sehemu ya barabara na siyo daraja lenyewe la Mpiji.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimesababisha madhara kadhaa kwa upande wa miundombinu ya barabara. Waziri Magufuli ameendelea kutahadharisha kuhusu shughuli za uchimbaji wa mchanga zinazofanywa karibu au chini ya madaraja, kwamba kwa maeneo mengi ndicho chanzo cha mito kuhama kutoka katika njia yake ya asili na kubomoa barabara. “Kama manavyoona daraja lenyewe ni zima na linauwezo mkubwa wa kupitisha maji lakini mto umehama kutokana na uharibifu wa mazingira” alisistiza Mhe. Magufuli.

Daraja la Mpiji lilifunguliwa rasmi mwezi Julai 2005 na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

TANROADS kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za SKOL na Estim Construction Company Limited zote za Dar es Salaam tayari wameanza kazi za kurekebisha sehemu hiyo.
Sehemu ya barabara iliyoomole katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wiara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe (aliyenyoosha mkono). Kulia ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele wa kwanza kulia) akiongozana na Viongozi wengine wakati walipotembelea kukagua sehemu ya barabara iliyobomoka katika barabara ya Dar – Bagamoyo. Wengine kutoka kushoto ni; (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam) Suleiman Kova, (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) Mhe. Said Mick saddik na (Mbunge Mteule wa Chalinze) Mhe. Ridhiwan Kikwete.
 
 
 
 
 

Related Posts:

  • Hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA-TAIFA;Mh. Mbowe Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimefanya mkutanmo wake mkuu wa Baraza kuu la Uongozi Mjini Doma siku ya Ijumaa. Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alihutubia mkutano huo     &nbs… Read More
  • Mume amuua Mkewe kwa Risasi    DCP Ahmed Msangi  Mwanamume mmoja mkazi wa Mahina wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemuua mkewe kwa kumpiga risasi na yeye mwenyewe kujiua baada ya kutokea ugomvi baina yao. Kamanda wa Polisi Mkoa… Read More
  • Pokea mwezi mtukufu wa Ramadhani   Assalamu alaykum warahmatullah Taara wabarakatu. Karibu katika darasa la Qur - an katika kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ikiwa leo ni Tarehe 2 Ramadhani, tunakukutanisha na Al Ustaadh Mohd Shraf Fama kutoka … Read More
  • Qaswida: Thola - al - Badru -Nasheed Arabic Assalam - araykum warah matullah, Tumekuletea Qaswida maarufu na inayopendwa na wengi hasa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Qaswida hii ineumbwa katika Lugha ya Kiarabu. Inaitwa Thola al badru alaina   &nb… Read More
  • John Bocco Out Azam FC John Bocco Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC ya Tanzania John Bocco ameachana rasmi na klabu yake hiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu kwa mafani… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE