April 14, 2014

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ameanza kampeni kanisani kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi. 
Alisema hayo jana katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Katika hotuba yake, Lukuvi aliwaeleza waumini waliofurika katika ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu wa kanisa hilo katika jimbo kuwa waendelee kuliombea Bunge lifanye uamuzi sahihi wa serikali mbili.
Aliwataka Watanzania kuipuuza Rasimu ya Katiba katika suala la Muungano na Serikali tatu kwa madai kuwa kutaka kuwapo mfumo huo ni kutaka Watanzania waingie vitani.
“Serikali tatu zikipita ni wazi kuwa hata makanisa yatafungwa kwani nchi haiwezi kuwa na amani tena, angalieni nchi ya Korea Kusini na Korea Kaskazini ambao waligawanyika na sasa ni maadui wakubwa wanaokaa mipakani wamenyoosheana bunduki,” alisema na kuongeza:

“Waumini ndugu zangu wapendwa, kwa sasa tupo katika hali mbaya sana hapo bungeni, tunaomba mtuombee kuna watu ambao wanataka madaraka kwa nguvu na wameanza kutafuta jinsi ya kuvunja Muungano na kudai kuwapo kwa Serikali tatu, nawaomba sana wapuuzeni wale wote ambao wanataka serikali tatu.”
 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE