May 04, 2014


Gosby
Gosby
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayesumbua na ngoma ya BMS na Monifere  ‘Gosby’  hatimaye amefungua milango kwa wasanii wenzake wa Bongo Fleva baada ya kuwa msanii wa kwanza kupata kibali cha kumiliki akaunti ya VEVO, kufuatia menejimenti yake kufanya kazi ya ziada na hatimaye kuweza kufanikisha zoezi hilo.
Alisema walifanya kazi kubwa kuhakikisha anapata akaunti hiyo licha ya usumbufu wa hapa na pale aliokuwa akiupata ukiwemo wa kuchelewa kurudishwa kwa majibu ya fomu twalizokuwa wakipewa na mtandao huo na hivyo  kuchukua muda mrefu kidogo kurejeshea  majibu.

Vevo 
”Menejimenti yangu ilikuwa inahangaika kupata Vevo kwa muda mrefu hata kabla sijatoa BMS, Prosesi ilikuwa ngumu, kwa sababu ulikuwa unawatumia jamaa vitu alafu wanakujibu baada ya kama miezi minne mitano, kulikuwa na fomu za kujaza kama nane au kumi ambazo kila moja jamaa walikuwa wanajibu, prosesi yake ilikuwa ndefu” alisema Gosby alipokuwa akifanyiwa mahojiano na  Clouds Fm
Kwa wale wasiyoifahamu Vevo ni mtandao unaotoa huduma ya  video ambao  unaomilikiwa na kuendeshwa kwa ubia wa lebo kubwa mbili ikiwemo ya Universal Music Group(UMG) na Sony Music Entertainment (SME), ikishirikiana na Google pamoja na Abu Dhabi Media.

           

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE