Msanii
nyota wa kike wa muziki wa kizazi kipya nchini, Khadija Shaban maarufu
kama ‘Keisha’ amejifungua mtoto wa kiume siku ya Jumatatu (Mei 5) katika
hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni.
Akizungumza
na Bongo5 leo Keisha,amesema anashukuru Mungu amejifungua salama na
mtoto anaendelea vizuri. “Nimejifungua mtoto mwingine wa kiume katika
hospitali ya Mount Mkombozi Kinondoni. Namshukuru Mungu nimejifungua
salama na mtoto anaendelea vizuri,” amesema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment