
Kutokana na mjadala wa bajeti ya wizara ya mambo ya nje uliokuwa
unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy ameporomosha matusi mazito
kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila mara wanalialia tu
kuwa wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na wakati
hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa
waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu.......
Alienda mbali zaidi kusema kuwa Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo
kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi wote wanakusanyika ila bado
wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio haki , na pia hata
umeme hawalipi na maji pia .
jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM ndugu Chombo , kuomba muongozo na
Kumtaka naibu Spika a mwambie Kessy kamwe asikanyage Zanzibar , hii
ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu , na alisema ni bahati mbaya kwa
CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu ......
Ndugai muda muda wote alikuwa akicheka , sijui nini maana yake .."...
0 MAONI YAKO:
Post a Comment