Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY"katika viwanja vya hosptali ya wilaya ya Hai. |
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" wakati wa kutangazwa kuwa mabalozi wa UNICEF. |
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua ya uteuzi Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu ya kuteuliwa kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto. |
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" ya kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto. |
Mabalozi
wa UNICEF ,Faraja Kotta Nyalandu na Ambwene Yesaya "AY wakijadiliana
jambo muda mfupi baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa UNICEF katika
kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
|
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akizungumza mara baada ya kuteuliwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto. |
| ||
Katika
kusherehekea siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni, Halmashauri ya
Wilaya ya Hai, ikishirikiana na viongozi wa serikali, UNICEF na Save the
Children, imezindua Kituo cha Huduma Jumuishi, kitakachowasaidia
wanawake na watoto ambao wameathiriwa na ukatili.
“Katika
kituo hiki, huduma za kuwasaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia na
ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni pamoja na huduma za afya, msaada wa
kisaikolojia, ulinzi/usalama na msaada wa kisheria vinaweza kutolewa
hapo katika eneo moja ndani ya kituo cha afya zikiwa zimeratibiwa vizuri
Zaidi,” alisema Charles Pallangyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii.
Aliongeza,
“kituo hiki kitasaidia kupunguza madhara zaidi ya ukatili kwa sababu
wahanga wa ukatili wataweza kupata huduma zote muhimu katika eneo moja
na hawatakuwa na sababu ya kurudiarudia kuwaeleza watoa huduma
mbalimbali walio katika maeneo tofauti yale mambo mabaya waliyoyapitia,
au kutakiwa kwenda na kurudi kutokana na ukosefu wa uratibu na uwezo wa
watendaji wa sekta mbalimbali katika kuwahudumia wahanga wa ukatili kwa
ukamilifu.”
Mwakilishi
wa UNICEF Tanzania, Dk. Jama Gulaid, anaamini kuwa kama tukifanya kazi
kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine, tunaweza kupata suluhu
katika kumaliza ukatili dhidi ya watoto. “Ukatili dhidi ya watoto uko
kila mahali na hatuwezi kuendelea kuufumbia macho. Watoto wote hapa
Tanzania wanahaki ya kuishi na kukua katika mazingira yasiyo na ukatili.
Kama sisi sote tukifanya kazi kwa kushirikiana pamoja, sina shaka
tutaweza kumaliza ukatili dhidi ya watoto.”
Katika
tukio hili huko Hai, UNICEF Tanzania imemteua msanii mahiri wa bongo
flava Ambwene Yessyah, anayejulikana zaidi kama AY, pamoja na aliyewahi
kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wao katika
‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto.’ Wote wameahidi
kusaidia kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’ na
wameonyesha kuhamasishwa na heshima hii waliyopewa kutoa sauti zao
kutetea ulinzi wa mtoto.
“Nimepewa
heshima kubwa kwa kuteuliwa kwangu kuwa Balozi wa UNICEF Tanzania na
nitajitoa katika kutumia sauti yangu na umaarufu wangu kusaidia
kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa Tanzania,” alisema AY alipokuwa
akikubali wadhifa huo.
Kwa
kuwateua AY na Faraja Kotta Nyalandu kama Mabalozi wa UNICEF Tanzania
wa kampeni ya ‘Kampeni ya Tokomeza Ukatili Dhidi ya Watoto’, UNICEF
inategemea kuongeza uzito na muonekano zaidi wa suala la ulinzi wa mtoto
katika mijadala inayoendelea kuhusu ukatili dhidi ya watoto na
kuonyesha kuwa kuna suluhisho la tatizo hili.
Kama
mwazo wa kazi yao katika shughuli za UNICEF Tanzania, AY na Faraja
Kotta Nyalandu walitembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika kituo cha
Polisi cha Hai kuona wenyewe kazi inayofanywa kusaidia wanawake na
watoto waliofanyiwa au kuathiriwa na ukatili.
Utafiti
juu ya Ukatili Dhidi ya Watoto, uliozinduliwa na Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto mwaka 2011, unaonyesha mambo yanayopelekea
uhatarishi wa watoto kwenye ukatili kimwili na kingono hapa Tanzania –
wastani wa msichana 1 kati ya 3 na mvulana 1 kati ya 7 wamefanyiwa
vitendo vya ukatili wa kingono, na zaidi ya asilimia 70 ya wasichana na
wavulana wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili kabla hawajafikia
umri wa miaka 18. Hata hivyo, wahanga wengi hawajamwambia mtu yeyote
ukatili waliofanyiwa na ni kesi chache sana zimefikishwa polisi.
Kumekuwa
na maendeleo katika kuboresha hali hii. UNICEF inasaidia serikali ya
Tanzania kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii kuanzisha na kuboresha ‘mifumo
ya Ulinzi wa Mtoto’ katika halmashauri 13.
Katika
halmashauri hizi, afya, ustawi wa jamii, polisi, sekta za elimu na
mahakama, magereza, wanasheria, asasi za kiraia pamoja na mifumo ya
kijamii isiyo rasmi wanaunda Timu ya Halmashauri ya Ulinzi na Usalama wa
Mtoto na wanashirikiana kuhakikisha kuwa kesi za ukatili wa watoto
zinashughulikiwa vyema na pia wanazuia ukatili kwa kuongeza uelewa wa
jamii juu ya ukatili dhidi ya watoto.
Lengo la Idara ya Ustawi wa Jamii ni kupanua utaratibu wa mfumo huu katika halmashauri 30 ifikapo mwaka 2016.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini
0 MAONI YAKO:
Post a Comment