
Kufuatia kifo cha mtoto Nasra, almaarufu kama ‘mtoto wa boksi’, kuna
kila dalili kwamba kifo chake kimetokana na maradhi aliyoyapata wakati
akiwa anaishi kwenye boksi. Kwa kuwa imethibitika kwamba mtoto alifariki
kutokana na ugonjwa wa pumu—kufuatia kufungiwa kwenye mazingira
machafu, kutoogeshwa na kupigwa na baridi masaa 24, na kwa kuwa wahusika
waliokuwa wakimfanyia ukatili huo tayari walishakamatwa na kufunguliwa
mashitaka ya kula njama za kumtesa mtoto huyo mdogo asiyekuwa na hatia
na asiyeweza kujitetea, mawakili wanaosimamia kesi hii watabadilisha
masitaka ya kesi na kuwa KESI YA MAUAJI YA KUKUSUDIA.
Adhabu kwa mtu anayeua kwa kukusudia ni KUNYONGWA MPAKA KUFA. Kwa hiyo,
wahusika wanasubiri kunyongwa hadi kufa pindi hukumu ya kesi hii
itakapotoka. Na kwa kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani hawa
wanadamu wasokuwa na haya, wajiandae kupokea kitanzi ili liwe fundisho
kwa washenzy wengine wenye tabia za kinyama kawa hawa wendawazimu.
NIONAVYO:
Natoa wito kwa watanzania wenzangu kutoa taarifa polisi haraka pindi
waonapo ukatili wowote dhidi ya wanyonge, hasa watoto wadogo, ili sheria
ichukue mkondo wake. Tatizo la watanzania walio wengi ni kwamba
hatujaliani. Unaweza ukamuona mzazi/mlezi akimtesa mtoto lakini ukakaa
kimya. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki yule kiumbe anayeonewa au
kunyanayaswa. Tuweni na huruma kwa viumbe hawa wa mwenyezi Mungu
wanaoonewa bila sababu za msingi huku wakiwa hawawezi kujitetea kwa
namna yoyote ile. Tukio la mtoto Nasra, ambaye Mungu amemuita kwake,
liwe fundisho kwa watu wengine wanaofumbia macho ukatili kwa watoto na
wanyonge.
Nawasilisha.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment