Waziri wa nchi, ofisi ya makamu wa rais (mazingira) Binilith Mahenge.
Vijana nchini Tanzania wametakiwa kushiriki kikamilifu katika suala la usafi wa mazingira kwa kuwa wao ndio wanauwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwa kukataa uchafu katika maeneo wanayoishi.
Wito
huo umetolewa leo jijini Dar-es-Salaam na vijana kutoka vikundi
mbalimbali ambao wameshiriki kufanya usafi wa mazingira katika maeneo
kadhaa ya jiji la Dar-es-Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku
ya mazingira duniani hii leo.
Wakizungumza kwa pamoja Vijana hao Bw. Charles Lupiliani ambaye pia
ni afisa wa bodi ya utalii mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Oyite Tungaraja
kutoka shirika lisilo la kiserikali la Voice Giving wamesema vijana wana
wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira ni jukumu lao ambalo
wanastahili kulipa kipaumbele ili kuepukana na magonjwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment