July 02, 2014


 
BAADHI ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wamelalamikia bei kubwa za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwenye badhi ya masoko jijini humo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi wa jiji hilo Bw. Khamis Mshaka na Bi. Salma Jumbe, walisema baadhi ya wafanyabiashara wanapandisha bei ya vyakula ili kupata faida.

Walisema hali hiyo inawafanya wananchi wengi hasa wenye kipato kidogo washindwe kumudu bei za vyakula wanapokwenda sokoni.

“Tabia hii si nzuri na imekuwa ikijitokeza mara kwa mara unapofika wakati wa mfungo...bidhaa zilizopo sokoni si za Waislamu pekee, hivyo tunaziomba mamlaka husika zichukue hatua,” walisema.

Bi. Jumbe alisema, baadhi ya wafanya biashara wanaficha vyakula kwenye maghala ili siku zinavyozidi kwenda, waviuze kwa bei kubwa jambo ambalo serikali inapaswa kulifanyia uchunguzi ili kukomesha tabia hiyo.

Kwa upande wake, Bi.Maria Albert ambaye ni mamalishe, anayefanya biashara ya kuuza chakula kwenye Mtaa wa Kongo, Kariakoo, alisema kutokana na bei kubwa ya vyakula, wanashindwa kupata faida.
Alisema bei ya sasa kwa mhogo mmoja ni kuanzia sh .1,000 kutokana na ukubwa wake ambapo magimbi ni sh. 3,000 kwa sado moja tofauti na awali ambapo ilikuwa ni sh.1, 500.

Naye Bw. Brown Sanga, mfanyabiashara wa nafaka katika Soko la Kisutu, alisema ni dhambi kupandisha bei za vyakula katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani.

“Wafanyabiashara tunapaswa kuwa na ubinadamu hata kama tunatafuta pesa, tunatakiwa kusaidiana ili ndugu zetu Waislamu tusiwaweke katika mazingira magumu ya kutafuta futari,” alisema.

Related Posts:

  • MARKEL: TUTAWALINDA WAYAHUDI NA WAISLA,U UJERUMANI Kansela Angela Merkel   Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameahidi kuwalinda Wayahudi na Waislamu wanaoishi nchini Ujerumani dhidi ya ubaguzi. Amesema demokrasia ndiyo njia bora ya kupambana na machafuko yanayo… Read More
  • ESCROW YAWAFIKISHA WENGINE MAHAKAMANI LEO HII   MZIMU wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, limeendelea kuwatafuna watuhumiwa  wa uchotwaji wa  mabilioni ya fedha za akaunti hiyo baada ya watuhumiwa wengine watatu kupandishwa mchana wa leo kizimban… Read More
  • MWANA BLOG HOI KWA KIPIGO Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine  Saudi Arabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake. Mwanablogu huyo ambaye pia ni… Read More
  • HUU NDIYO MPANGO MPYA WA THT 2015            Imezoeleka Tanzania House of Tallent (THT) imekua ikitoa wasanii peke yake ambao asilimia kubwa ya wasanii wengi wa Bongo Fleva wamepitia kwenye mikono ya Nyum… Read More
  • MAMA AMCHARANGA VIWEMBE MWANAE WA KUMZAA Mama mzazi aliyetajwa kwa jina la Feromena, mkazi wa Meko-Mtongani, Kunduchi jijini Dar, anatuhumiwa kumcharanga viwembe mwanaye wa kumzaa aliyetajwa kwa jina moja la Zena mwenye umri wa miaka kumi Kwa upande wake mama … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE