July 10, 2014

Sudan Kusini bado inakabiliwa na hali tete licha ya mkataba wa amani kutiwa saini
Inaripotiwa kuwa China imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 38 nchini Sudan Kusini licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo ambao huenda utaitumbukiza katika baa la njaa.
Nyaraka zilizogunduliwa na wataalamu wa masuala ya ulinzi zinaonyesha kuwa makombora, bunduki za rashasha na risasi viliwasili nchini Sudan Kusini mwezi uliopita kupitia bandari ya Mombasa nchini Kenya.
Wanadiplomasia wanakadiria kuwa Sudan Kusini inatumia mamilioni ya dola kwa ulinzi.
Kwingineko, muungano wa ulaya umewawekea vikwazo viongozi na kupiga tanji mali ya wakuu wa kijeshi wa nchi hiyo kwa tuhuma za kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ambayo yangeleta mazingira ya amani na kuziia mauaji ya maelfu ya wanachi.
Baraza la Muungano huo, halikuwataja wawili hao katika taarifa yao wala kutaja pande wanazounga mkono.
Marekani imechukua hatua sawa na hizo dhidi ya viongozi kutoka pande zinazozozana.
Vita vilizuka mjini Juba Disemba mwaka jana kati ya serikali na wapiganaji wa aliyekuwa makamu wa Rais Riek Machar.
Mgogoro huo bila shaka umetonesha kidonda katika taifa hilo changa zaidi duniani tangu kujitawala mwaka 2011.

LIKE PAGE YETU KATIKA  FACE BOOK BOFYA  UBALOZINI RESPECT

Related Posts:

  • Rais mpya wa Ufaransa aapishwa   Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, anaapishwa hivi sasa, juma moja baada ya kupata ushindi mkubwa katika marudio ya uchaguzi mkuu wa Urais nchini humo. Alimshinda pakubwa kiongozi wa chama cha kulia Bi Marin… Read More
  • Ashikiliwa na Polisi kwa kumuua mumewe kisa wivu   MKAZI wa Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadija Mbarouk (44), anashikiliwa na polisi kwa madai ya kumuua mumewe kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. Mtuhumiwa huyo inadaiwa alimchom… Read More
  • TRA Wakana kuhsu Ml 400 za Diamond Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandi… Read More
  • Shambulizi la uhalifu wa mtandao laathiri mataifa 99 duniani   Sambulizi la kihalifu mitandaoni lililotendeka kupitia utumizi wa vifaa vinavyoaminika kuibwa kutoka kitengo cha ujasusi nchini Marekani NSA limeathiri mashirika tofauti duniani. Kampuni ya kulinda uhalifu wa mi… Read More
  • Lowassa achukizwa na serikali ya Dar   Mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mh. Edward Lowassa amelaani vikali kitendo cha serikali ya Mkoa wa Dar es salam kuzuia kongamano la demokrasia lililopangwa kufanyika siku ya leo may 1… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE