Mrisho-Ngasa-in-on-of-Taifa-Stars-matches
DURU za habari zinaeleza kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzaniam Taifa stars, Mholanzi, Mart Nooij amemuondoa winga machachari wa timu hiyo na klabu ya Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa `Anko` katika kikosi kitakachopepetana na Msumbiji `Black Mambas`. Imeelezwa kuwa Nooij amefikia maamuzi hayo baada ya Ngassa kushindwa kuripoti katika kikosi chake siku kilipojipima ubavu dhidi ya Botswana na kulala mabao 4-2, mjini Gaborone. Kabla ya mechi hiyo, kocha Nooij alimuita Ngassa, lakini alikaidi na kwenda Bondeni, Afrika kusini kufanya majaribio na klabu inayoshiriki ligi ya huko, Free State Stars ambako alifuzu, lakini uhamisho umekuwa mgumu. Ngassa baada ya kufuzu majaribio, klabu ya Free state ilitangaza kutuma ofa ya dola elfu 80 sawa na milioni 130 za Kitanzania, lakini inasemekana Yanga waligoma. Hata hivyo uongozi wa Yanga kupitia kwa katibu mkuu, Beno Njovu alisema kuwa Free State hawajafika mezani kuzungumza nao bali wanasikia kwenye vyombo vya habariCHANZO SHAFII DAUDA
0 MAONI YAKO:
Post a Comment