July 06, 2014

 


Kocha wa Uholanzi Luis van Gaal amesema urefu wa kipa Tim Krul ndio ulimfanya amchezeshe katika mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Costa Rica.
Krul, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, (mita 1 sentimita 93) aliingia badala ya kipa aliyeanza Jasper Cillessen zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya mikwaju ya penati kuanza kupigwa. Jasper ana urefu wa futi 6 inchi 2 (Mita1 sentimia 87).
Krul aliweza kupangua penati mbili, na hivyo Uholanzi kushinda kwa magoli 4-3.
"Tulidhani kuwa TIm ndio kipa bora wa kuzuia penati," alisema Van Gaal. "Ni mrefu na ana nafasi zaidi ya kuzuia."
Menenja huyo wa Manchester United aliongeza kusema: "Ilifanikiwa, ilienda vyema. Ninajivunia kidogo kwa hilo."
Uholanzi, timu pekee kati ya nne zilizosalia ambayo haijawahi kushinda Kombe la Dunia, itapambana na Argentina mjini Sao Paulo siku ya Jumatano. Brazil itacheza na Ujerumani katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumanne.

Related Posts:

  • Ngassa ajutia nafasi, ailalamikia Yanga   Na Richard Bakana, Dar es salaam MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mrisho Ngassa, amejutia uamuzi wake wa kukataa kujiunga na El Merreikh ya Sudan akisema kuwa yalikuwa ni… Read More
  • Picha za Wema Sepetu na Ommy Dimpoz, zilipigwa usiku wa manane    Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hak… Read More
  • Cindy Sanyu amponda Miss Uganda live   Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Cindy Sanyu ameibua mjadala mzito mtandaoni baada ya kufunguka wazi kuwa mrembo anayeshikilia taji la miss Uganda kwa sasa, Leah Kalanguka ana muonekano mbaya, na kukazia … Read More
  • UN yailaumu Tanzania kwa hali ilivyo DRC   Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu Tanzania kwa kuwaruhu… Read More
  • Samsung yakiri Tv zao zinanasa sauti    Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE