Ile ahadi aliyoiahidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Kikwete leo imetimia baada ya wasanii mbalimbali wa filamu na waimbaji
wa muziki kutoka kwenye aina tofauti ya muziki ikiwemo waimbaji wa
Bendi,nyimbo za Injili na Bongo Fleva.
Terrence J,Chaka Zulu na David Banner ndio walikua waongozaji wa
semina hiyo ambayo ilianza saa 4 asubuhi na kumalizika jioni saa 11 na
nusu July 14,miongoni mwa wasanii waliiopata nafasi ya kuongelea
changamoto za muziki wa Tanzania ni pamoja na Khadija Kopa.
Khadija Kopa amesema muziki wa Tanzania una changamoto nyingi na
kusema ili kuwe na mafanikio kwenye sanaa yetu ya Tanzania kuna umuhimu
wa wasanii wote kuwa na umoja ndipo mengine yatafuata na kuwa rahisi.
Wadau hao wamekuja nchini kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa
muziki na filamu ili kuweza kujiingizia kipato kupitia kazi zao na
kujitangaza zaidi kimataifa,semina hii imefanyika kwenye ukumbi wa BOT
uliopo Posta Dar es salaam.
Hizi ni baadhi ya picha za semina hiyo.
Malkia wa mpasho Khadija Kopa
Mpoto
Dayna Nyange na Tarrence j
Nando
TARRENCE J NA CHAKA ZULU
Boss Ruge Mutahaba
Ally Kiba
Mzee Yusuph
0 MAONI YAKO:
Post a Comment