Mtu mmoja amefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu mjini Arusha Tanzania.
Polisi wamewakamata wayu wawili wakihusishwa na shambulio hilo lililotokea kwenye mgahawa wa 'Vama Traditional Indian cuisine' jijini Arusha Kaskazini mwa Tanzania.
Watu wasiojulikana walirusha bomu ndani ya mgahawa kupitia mlangoni ambapo watu wanane wamejeruhiwa moja kati yao akiwa na majeraha makubwa.Shambulizi hilo liliyokea siku ya jumatatu saa nne usiku.
Aidha,katika matukio mengine, jumla ya Watu 20 wanazuiliwa na Polisi wakiwemo watu sita wanaosadikiwa kujihusisha na mlipuko wa bomu uliotokea mkoani Arusha juma lililopita nyumbani kwa Kiongozi wa dini Sheikh Sudi Ally Sudi na kujeruhi watu wawili.
Polisi wanaendelea na upelelezi kuhakikisha inawatia nguvuni watu waliohusika na matukio hayo.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo
0 MAONI YAKO:
Post a Comment