Boss wa Manchester United Louis van Gaal anataka kumsajili kiungo wa
Juventus Arturo Vidal, 27, kwa mkataba wa pauni milioni 34 kiasi ambacho
kitafikisha pauni milioni 200 za kununua wachezaji Old Trafford katika
kipindi cha miaka miwili (Independent), United huenda wakamtoa Javier
Hernandez, 26, kwenda Juventus, katika mkataba wa Vidal (Daily Express),
Manchester United pia wanatarajia kutaka kumsajili Daley Blind, 24
kutoka Ajax kwa pauni milioni 18 katika siku chache zijazo (Sun),
Arsenal wanaonekana kuzidiwa kete na Roma, kumsajili beki wa kati Kostas
Manolas, 23 kutoka Olympiakos (Goal), Manchester United na Arsenal
wamepata matumaini ya kuendelea kumfuatilia beki wa Roma Mehdi Benatia,
27, baada ya klabu hiyo ya Italia kuvunja mazungumzo na Bayern Munich
(Daily Star), Arsenal huenda wakamfuatilia Danny Welbeck, 23, kutoka Man
United, au Loic Remy, 27, kutoka QPR kuziba pengo la Olivier Giroud
ambaye huenda akakosa kucheza kwa miezi mitatu kutokana na jeraha la
kiwiko cha mguu (Daily Telegraph), Southampton wameanza kumfuatilia beki
wa Atletico Madrid Toby Alderweireld, 25, na kuwazidi Monaco (Times),
Tottenham wapo tayari kutoa pauni milioni 8 kumchukua nahodha wa Sevilla
Federico Fazio, 27 (London Evening Standard) Chelsea wanazungumza na
Roma kumchukua Mattia Destro, 23 (Daily Mirror), QPR wanakaribia
kumsajili beki wa Liverpool Jack Robinson, 20 kwa mkataba wa pauni
milioni 1 (Daily Mirror), West Ham wamemuulizia beki wa kati wa Bayer
Leverkusen Philipp Wollscheid, 25, (Daily Mail), Sunderland, QPR na West
Brom wanamtaka kiungo wa Leicester Andy King, 25, (Sun), AC Milan bado
wanataka kumchukua Fernando Torres kutoka Chelsea, wakala wake
akipendekeza kumchukua kwa mkopo, ingawa mshahara wake mkubwa unaonekana
kuwa kikwazo (Metro), Napoli wataanza kumfuatilia tena kiungo wa
Tottenham, Sandro kwa mkopo (The Times), Sporting wamewaambia Arsenal
kuwa watakubali kitita cha euro milioni 30 kumsajili William Carvalho,
kama Arsenal watakubali kumtoa Serge Gnabry, Francis Coquelin au Yaya
Sanogo kwa mkopo (The Times), Everton wanakaribia kukamilisha usajili wa
Samuel Eto'o. Roberto Martinez alikuwa akimtaka Danny Welbeck wa Man
United, lakini alikatishwa tamaa na bei ya Pauni milioni 15 (The Times)
na boss wa Inter Milan, Walter Mazzarri amewaambia watu wake kuwa wako
huru kujaribu kumsajili Ezequiel Lavezzi kutoka Paris St-Germain
(Tuttosport). Zimesalia siku sita kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka wote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment