September 04, 2014

01JESHI la Polisi nchini limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kutuma ujumbe wa matusi, uchochezi, picha za utupu sanjari na kukashifu viongozi wa Serikali, dini na watu mashuhuri.02Akizungumza Dar es Salaam, Septemba 3,2014  Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema kuwa tayari baadhi ya watu wameshakamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na wengine wanaendelea kuhojiwa.

“Kumejitokeza tabia kwa baadhi ya watu kutumia mitandao ya kijamii na simu za kiganjani kinyume na malengo yaliyokusudiwa kwa kusambaza taarifa za uchochezi, kashfa,kuchafua viongozi wa Serikali.
 “Wengine wamekuwa wanasambaza picha utupu ambazo hazina maadili, hali ambayo ni kosa la jina, ingawaje mwingine anaweza hasijue kuwa kufanya hivyo ni kosa lakini sheria haitamuacha, alisema.
 Senso aliendelea kubainisha kuwa kuvunja kutofahamu sheria kwa kutoifahamu si sehemu ya kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria, atakabainika kutenda kosa hilo bila kujali anaifahamu sheria au la, atachukuliwa adhabu kali.
 Alisema oparesheni ya kuwabaini wanaosambaza ujumbe zinaendelea nchi nzima kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa lengo la kuwakamata waharifu wa aina hiyo.
 Aliongeza kuwa hatua hiyo pia inawatia hatiani wale wote wanaotumia mitandao kufanya utapeli na kujipatia kipato kwa watu mbalimbali nchini sanjari na blogs zinazosambaza picha chafu ambazo ni kinyume na maadili.
“Wapo baadhi ya watu wanatumia mitandao ya simu kutapeli watu na kujipatia kipato, hivyo nao ni sehemu ya waharifu wanaotafutwa na jeshi la polisi na yeyote atayekamatwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yake,” alisema.
 Hivyo alisisitiza kuwa Jeshi hilo linatoa onyo kali kwa watu kujiepusha na uharifu huo, na kuwataka wale wanaotumiwa wa aina hiyo kutousambaza kwa wengine bali waufute.
 Pia aliziomba kampuni za simu za mkononi pindi wanapoona ujumbe wa aina hiyo wasiruhusu uende kwa mwingine ili nao wawe sehemu ya kupambana na uovu huo.

Related Posts:

  • Baby Madaha kuja na Corazon Msanii wa muziki na mwigizaji, Baby Joseph Madaha, ‘Baby Madaha’ baada ya ukimya wa muda mrefu amejipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Corazon’. Madaha amesema kwa sasa anamalizia video ya wimbo huo ambao picha zake … Read More
  • Anayetuhumiwa kumtukana Rais Magufuli amepata dhamana     Baada ya Mahakama ya hakimu mfawidhi Arusha kukaa chini na kupitia hoja mbili zilizotolewa na upandea wa mashtaka na mshitakiwa Mahakama imeridhwa ia kutoa dhamana … Read More
  • Muuaji aua watu 182   Waziri wa mawasiliano Getachew Reda Wananchi wa Ethiopia wameeleza namna muuaji wa watu zaidi ya 182 kuwa alikuwa ameshikilia bunduki na ni raia wa Sudan Kusini upande wa Magharibi mwa Gambela mk… Read More
  • Karibu katika Magazeti ya leo Jumatatu April 18     Habari za leo hii jumatatu ya 18 April 2016. Karibu mpendwa katika kurasa za magazetini leo hii. Tumekuwekea kurasa zilizobeba uzito katika magazeti ya leo jhii. Kupata habari kwa undani fika katika meza za … Read More
  • Zifahamu siri saba za ‘smartphone’ ambazo hukuzifahamu MATUMIZI ya simu za kisasa (smartphone) yamezua maneno na uvumi wa kila aina katika blogu, magazeti mbalimbali, barua-pepe, mitandao ya WhatsApp na Facebook, hata hivyo, mtumizi wa simu hizi hatakiwi kua… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE