September 24, 2014

 
Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
 Stori:Shani Ramadhani, Issa Mnally na Gabriel Ng’osha
“MADAM...Madam...Madam...” ndizo kelele zilizosikika wakati Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ alipokuwa akimtunza fedha nyingi dogo machachari wa Bendi ya Yamoto, Asilahi Isiyaka ‘Dogo Aslay’.
Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.
MAMBO YALIVYOANZA
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza, ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.

“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo gani,” alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza.
 
Aslay akifurahiya minoti aliyomwagiwa na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.
ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa huku akiishia kuzitazama bila kuimba chochote.

BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha ndipo akaacha na kushuka jukwaani.


Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa na marafiki zake.
KWA NINI ASLAY TU?
Wakati zoezi hilo likiendelea, kuna baadhi ya mashabiki waliibua minong’ono wakihoji kwa nini atunzwe Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso, Enock na Beka?
“Mbona kama anampendelea Aslay tu  wengine hawatunzi ona hela zote ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure, haikatazwi lakini,” alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia shoo hiyo.

 
MPAMBANO UNAENDELEA!
Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya tukio kama hilo katika Ukumbi wa Thai Village Masaki kwa kumtunza ‘pesa ndefu’ mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko ‘vizuri’ kifedha.

Related Posts:

  • New Music: Linah – Imani   Msanii Linah ameachia wimbo mpya unaitwa “Imani” umetaarishwa na Producer Nash Designer ni wimbo ambao unaujumbe mzuri sana sikiliza hapa alafu toa maoni yako. … Read More
  • Kutoka katika kurasa za Magazeti ya leo Jumatano 11 Mei 2016     Habari za Asubuhi mpenzi msomaji, karibu katika kurasa za magazeti leo hii. makubwa yaliyoandikwa ni haya                       &n… Read More
  • Tahadhari Kuhusu Makachero FEKI Wa TAKUKURU   Tangu kuanza kwa zoezi la kufuatilia wafanyabiashara wanaoficha sukari kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Dr John Pombe Magufuli, kumekuwa na wimbi la watu wanaojiita “makachero wa TAKUKURU  kuto… Read More
  • AY, FA waenda Kortini Kuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao. Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania a… Read More
  • Orodha ya Mataifa fisadi zaidi Afrika Mashariki   Baada ya waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kunaswa na kamera akiidunisha Nigeria kuwa mafisadi wakuu kote duniani BBC imeamua kuangazia kwa umakini ikiwa matamshi hayo ni ya kweli. Je Nigeria imeorodhes… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE