
Chanongo wataendelea kupumzika. Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku kwamba, Tambwe alifanya mazoezi vizuri jana na ameonyesha yuko fiti kabisa. Tambwe aliumia goti juzi jioni mazoezini Uwanja wa Boko Veterani na kuzua hofu kwamba anaweza kuongeza idadi ya majeruhi wa timu hiyo ambayo tayari inawakosa Ivo Mapunda, Paul Kiongera,
Nassor Masoud ‘Chollo’, Baba Ubaya na Chanongo. “Tambwe amefanya mazoezi vizuri tu, kama nilivyosema, hayakuwa maumivu makubwa na tunashukuru imekuwa hivyo. Ni matarajio yetu ataanza mechi na Stand,”amesema. Daktari huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar amesema kwamba Issa na Chanongo wameendelea na mazoezi mepesi na kwamba hawatakuwa tayari kwa mchezo wa
leo. Baada ya sare mbili mfululizo 2-2 na Coastal Union ikitoka kuongoza 2-0 hadi
mapumziko na 1-1 na Polisi Moro pia ikiongoza hadi baada ya kipindi cha kwanza, Simba SC itajaribu kusaka ushindi wa kwanza leo dhidi ya timu iliyopanda msimu
huu, Stand. Tayari Stand wamekwishaonja ladha ya ushindi katika Ligi Kuu kufuatia kushinda 1-0
katika mchezo wao uliopita dhidi ya wenyeji Mgambo JKT mjini Tanga. Lakini ikumbukwe Stand ilianza na kipigo cha nyumbani cha mabao 4-1 kutoka kwa Ndanda waliopanda nao Ligi Kuu msimu huu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment