November 14, 2014


 
Rais Jakaya Kikwete ametoka wodini katika Hospitali ya Johns Hopkins na kuhamishiwa kwenye hoteli maalumu ambako ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.
Rais Kikwete alifanyiwa upasuaji wa tezi dume wiki iliyopita na afya yake imekuwa ikiimarika siku hadi siku.

Makundi mbalimbali ya wananchi yamekuwa yakimtakia uponaji wa haraka kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu. Miongoni mwa waliomtakia afya njema ni familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambayo imeeleza kupokea kwa masikitiko taarifa za kuugua kwake na kumwombea apone haraka ili aendelee na majukumu yake kwa Taifa.

Chama cha RPP cha Rwanda kimemtumia salamu za pole Rais Kikwete na kuungana na mamilioni ya Watanzania kumwombea ili arejee katika afya yake na majukumu ya kila siku.

“RPP tutashirikiana na familia, marafiki na mamilioni ya Watanzania kumwombea Rais Kikwete aweze kupona haraka. Rais Kikwete ni jirani yetu na mtetezi mkubwa wa kanda hii katika kupata ukombozi wa kijamii, kisiasa na kiuchumi,” ilisema taarifa ya RPP kwa umma iliyotolewa na Rais wa chama hicho, John V Karuranga.

Aondoka wodini

Wakati Rais Kikwete akiondoka wodini, alikuwa anatembea akiwa amesindikizwa na daktari bingwa, Edward Schaeffer kutoka Hospitali ya Johns Hopkins na mkewe Salma.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa juzi ilisema: “Afya yake imekuwa inaimarika kiasi cha kuanza mazoezi ya kutembea na akiwa katika hoteli hiyo, ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari.”

Iliongeza: “Rais Kikwete ataendelea kupatiwa matibabu, kutembelewa mara kwa mara na madaktari na kuwa chini ya uangalizi wa wauguzi muda wote. Wiki moja baadaye, Rais Kikwete atafanyiwa tathmini ya kuwawezesha madaktari kuamua hatua inayofuata ya matibabu yake.”

Taarifa hiyo ilisema: “Kutokana na kuondolewa kwa bandeji kwenye mshono ambao nao umeanza kukauka vizuri, Rais Kikwete atakuwa katika hoteli maalumu (haikutajwa), iliyo na uhusiano na Hospitali ya Johns Hopkins.”

Related Posts:

  • Sterling apata mtetezi   Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ametetewa kwa kuwa na hamu kujiunga na vilabu vikubwa. Mshambuliaji huyo wa Liverpool huenda asilaumiwe kwa kuonyesha hamu ya kung'aa zaidi na kutaka kushinda vikombe. Hii ni kw… Read More
  • Mtu mmoja apigwa risasi    Habari kutoka Burundi zinasema kuwa mtu mmoja amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Bujumbura. Mtu huyo alikuwa miongoni mwa waandamanaji wanaopinga hatua ya rais Pierre Nkurunziza kugombea urais kwa aw… Read More
  • Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi   Burundi:Nkurunziza ahairisha uchaguzi  Rais wa Burundia Pierre Nkurunziza amehairisha uchaguzi wa ubunge kwa siku kumi . Msemaji wa rais Willy Nyamitwe ameiambia shirika la habari la AF… Read More
  • Watanzania watakiwa kudumisha amani   Viongozi wa dini, wanasiasa na wazee nchini wamewaonya Watanzania kujiepusha na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani. Viongozi hao walisema hayo, Dar es Salaam jana katika Mkutano kuhusu Amani na Utulivu wa T… Read More
  • Uganda wapo tofauti na sisi katika video: Mr Blue   Msanii Mr blue ambaye wiki mbili zilizopita alikuwa nchini Uganda kwa ajili ya kufanya video na msanii Navio kutoka Uganda alifunguka na kusema kuwa ameona tofauti kubwa sana katika ufanyaji wa video bongo na nch… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE