December 28, 2014

diva266 
Hellow Mpendwa 2014.
Dhumuni la barua hii ni kuandika kwa kiswahili kabisa ili tuelewane, ili nikushukuru na kukuambia ulishindwa na ulishinda vingine vyenye mafanikio pia, mfano kazi zangu za kijamii na kazi zangu binafsi kama mjasiriamali tukianzia na biashara zangu za accessories online na events zangu ambazo nimetengeneza ramani na pesa nzuri kwa matumizi yangu ya kimaisha alhamdulilah kila kitu kilikuwa sawa na kuna vingine havikuwa sawa 2014 yote nashukuru.
ulikuwa mwaka ambao ulipaswa kunimaliza kimaisha lakini ulishindwa, hukuwa na nguvu hio, ulichukua watu wangu muhimu maishani na kuniumiza vilivyo mapema mwezi wa kwanza, sijajua umenifundisha nini ila najua umenifundisha vitu ambavyo Pesa haviwezi nunua nayo ni Mapenzi. Umenifundisha kuwa mama yangu hatarudi tena hivyo niache ndoto za alinacha na kumlilia kila siku au nikiwa peke yangu sababu sitaweza muona hapa duniani, Umenifundisha kumuombea sana kama nifanyavyo kabla ya kulala, Bibi yangu pia, Bibi yangu nina mengi ya kukuambia lakini najua utakuwa unasoma hii blog au sijui vyovyote ila jua nakukumbuka sana kila siku, bibi ulinilea na ukanifundisha kufuata ndoto zangu ni wewe ndio uliona nitafanya hii kazi nifanyayo kabla hata sijatimiza mika 13,ulinidekeza sana sana sana labda ndio maana niko hivi nadekadeka…..au nanunanuna sababu najua ungekuwepo ungenibembeleza kama ulivyokuwa unafanya, ulinidekeza sana labda ulinipenda sana ikawa ilivyokuwa ukaniacha nikashindwa hata kulia sababu sikuwa naamini, sikulia bibi unajua ulivyoondoka nilikuwa nakuangalia ……nililia nilipoona mwezi umekatika na kweli hata sauti yako sikuisikia tena, nakumbuka vituko vyako Tanga, shamba na ulipokuwa unanisomea bible kila siku usiku, ulisema niamini Mungu kwa kila nifanyalo na ndio ninavyofanya, ulisema nisiwe na marafiki wa ovyo, ndio ninavyofanya, ulisema niiwe mpiganaji kweli na nisitegemee pesa za mtu yoyote bibi wewe ndio ninavyofanya… i miss you so bad…and yas droppin dis chozi kidogo na nitalifuta na kuendelea kuandika, yaan ulikuwa ni bibi bora maisha yangu yote nakupenda kweli bibi wajina wangu, gladly i have your heart….and your name as well , pumzika kwa amani….ila 2014….
2014 , 2014, 2014 nisemeje? maana nina mengi sana ila machache yatatosha. Umenifundisha nijue kuwajua watu wanaocheka ukiwa nao usoni na umenifundisha Kuwa watu hubadilika na wengine hawataki badadilika sababu wanasababu zao binafsi ila umenifundisha kuendelea kutabasamu hata kama mambo hayaendi sawa. Mpendwa 2014 umenifundisha kutochukia yoyote asiesawa sababu mimi pia siko sawa umenifundisha kutochukia wenye chuki binafsi na umenifundisha kusambaza upendo sababu hakuna atakaedumu milele lakini licha ya yote umenifundisha kusahau na kusamehe. Umenifundisha kujipenda zaidi na kuwa na furaha sababu furaha huanza kwako mwenyewe , umenifundisha kupambana na kuwa mvumilivu hata nikiandamwa vipi sababu kweli tatizo nyota na sijatetereka . Umenifundisha kuwa sio kila mtu ana moyo sawa na wako wengine wana mioyo iliojaa chuki, wivu, usenge-nyaaji na roho mbaya isio kifani. Umenifundisha kutokukata tamaa na kupigana na maisha bila kushindwa na bila mwengine kujua uko katika hali gani ya kimaisha. Nina furaha kusema kuwa nitakukumbuka sana sababu uko katika kitabu changu cha kumbukumbu kina jina lako najua hautarudi tena ila mabaya na mazuri yako yatabaki kwenye kichwa changu na nitaendelea kuheshimu kila ulilonifanya nijifunze tena kwa nafasi kubwa zaidi,toka chini ya moyo wangu na kwa undani kabisa na ukubwa usioelezeka nasema Asante 2014. Hukunifanya nikushangae ila umenifanya nijiweke tayari kwa ajili ya 2015 Inshaallah Kheir na Namshukuru Rabuka kwa kuwa bado ninapumua Pumzi yake nisio ilipia. Ni kwa rehema zake na nashukuru kwa Maisha mazuri alionijalia. Nitakukumbuka na nitakuenzi, nitakushukuru kwa kila baya na jema lako. Nakupenda sana 2014 na nitakupenda milele.
kuna wengi wa kuwashuru mpendwa 2014.. ila Mwaka 2014 unaisha .. and yas Jas Wanna Say Thanks To My Boyfriend… Mmhhh Boyfriend is My fave Word ryt now.. call him Baby, Hubby, his name Pia…… Thank you Darling. I am Grateful to have you .. grateful for le mbebez who knows Me better than anyone else on this Planet and Still loves me.. But what can a boyfriend Do?! i Cherish My time with You My Love, you are so serious about Creating Change in This Stub .. girl .. can see the way you Battling to change My Life and the way i live.. lol. take a Chill Pill Hun But Ey thanks for Making My Life what it is… can’t mention all but few… thanks for bringing different flavours of fun and adventure into Our Lives .. thanks for Teaching Me alot about Marketing.. learning so much .. last but nat least .. Thanks for Connecting with Me. Thank You Mchumba…thank you for Opportunities to grow, to develop and to serve . You Make My life Worthwhile. And Yo Truly My King. luhyuh babe. best Man yas My Man On Earth. My baby baby ❤️ lov you So Much Boo. and yas Kwenye Huba value and shikilia ulichonacho #Soul2Soul forever Thankful and I am Greatful, huwa nakukosea ila haya ya dunia tu uwe unanisamehe as no one is perfect ila forgive me bureee, but jas know nakupenda to pieces nakupenda to the moon and back,
dear 2014 nina mengi ila hayo yanatosha .
Wako katika ujenzi wa Mtandao wa kijamii
Diva Gissele.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE