
HABARI
zilizotufikia usiku wa kuamkia leo, zinasema kuwa Mshambuliaji wa timu ya Polisi
Moro, Danny Mrwanda, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Klabu ya
Yanga ya jijini Dar es salaam
Imekuwa
ni tofauti na mategemeo ya mashabiki walio wengi wa soka kutokana na
habari zilizozagaa kuanzia juzi kuwa mchezaji huyo 'eti' alikuwa tayari
ameshakamilisha taratibu zote za kujiunga na Klabu ya Simba, ambao
walimtaka na kufanya naye mazungumzo.

watani
wa jadi kufanyiana 'Kitu Umafia', mara kadhaa kwa kuchukuliana
wachezaji na kupandiana dau kama ilivyokuwa kwa baadhi ya wachezaji
akiwamo, Mbuyu Twite, na wengineo na ndivyo Yanga walivyofanya tena kwa
Mrwanda usiku huu.
Ikumbukwe
kuwa Simba, walikuwa wameshatangaza dau la kumsajili mchezaji huyo
katika kipindi hichi cha dirisha dogo na tayari taratibu zilikuwa
zimekwishaanza.
Chanzo
cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga
imeamua kumsajili Mrwanda ili kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi
aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa
ni majeruhi, na mshambuliaji pekee wa ndani aliyebaki tegemeo akiwa ni
Hussein Javu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment