Taarifa ambazo zilianza kusambaa kutoka kwa mashuhuda ni kwamba Wezi hawa walikua wakipiga watu, kupora vitu mbalimbali na hata kuharibu baadhi ya magari na pikipiki kwa kuvunja taa wakati wakipita kwenye mitaa mbalimbali.
Baada ya taarifa kusambaa Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alizungumza kwenye TBC1 na kusema hawezi kupinga uhalifu kufanyika leo mtaani lakini sio kwa kiasi hicho ambavyo imeripotiwa, yaani habari imekuzwa kuliko ukweli wenyewe.
Miongoni mwa aliekumbwa na huu mkasa ni mtangazaji wa Clouds FM Efphraim Kibonde kama ambavyo anasikika akizungumza kwenye hii sauti hapa chini.Pia mtayarishaji wa muziki wa Bongo freva Sheddy naye amekumbwa na mkasa huu
SAUTI YA KIBONDE
PRODUCER SHEDDY
0 MAONI YAKO:
Post a Comment