February 20, 2015

 
 Mjumbe wa baraza kuu la Uongozi CUF Taifa kutokea Morogoro Mjini Marala Maharagande kipenzi cha wana Morogoro, ameomba ridhaa ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao.
  Maharagande ambaye aliwahi kugombea nafasi hiyo kwa chama hicho mwaka 2005 na kuleta upinzani mkubwa sana kwa chama tawala, tayari ameandika barua ya maombi juu ya azma yake hiyo kufuatana na taratibu.


 Tayari wakazi wa  jimbo la Morogoro wameanza kurudisha matumaini mapya kwa Maharagande ambaye kwa asilimia kubwa amekuwa akikubarika sana jimboni humo. Tutamtafuta Maharagande na kuzungumza naye juu ya hili

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE