Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo kimesitisha uungaji mkono wake kwa vikosi vya
Kongo kwa ajili ya kuendesha oparesheni dhidi ya waasi wa Kihutu wa
Rwanda wa FDLR, kufuatia tuhuma dhidi ya majenerali wawili wa Kongo za
kukiuka haki za binadamu. Kikosi cha kulinda amani nchini Kongo DR
kimebainisha masikitiko yake kufuatia kuhusishwa majenerali wawili wa
jeshi la Kongo (FARDC) na ukiukaji wa haki za binadamu na kwa hiyo
kikosi hicho kimeamua kusimamisha msaada wake kwa jeshi hilo dhidi ya
oparesheni za kuwafurusha waasi wa Rwanda wa FDLR. Waasi wa FDLR
wanawajumuisha wanajeshi wa zamani wa Rwanda na wanamgambo wa Kihutu
waliohusika na mauaji ya kimbari nchini humo ya mwaka 1994, waasi ambao
kwa miaka kadhaa sasa wamekuwa wakisababisha machafuko katika eneo la
Maziwa Makuu la katikati mwa Afrika.
KATAMBI AMEKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WAJUMBE WA CCM SHINYANGA MJINI
-
Na; Mwandishi Wetu - DODOMA
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe...
2 hours ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment