March 18, 2015

 

Picha hii siyo halisi ya tukio  

Jeshi la Polisi mjini Tunduma mkoani Mbeya limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliofunga barabara.

Akiongea na East Africa Radio kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mbeya ACP, Ahmed Msangi amesema vurugu hizo zimetokana na mgogoro wa kiwanja baina ya chama cha Mapinduzi CCM na wananchi ambao wamekuwa waking'ang'ania kumiliki kiwanja hicho licha ya maamuzi ya mahakama kutaja CCM ndio mmiliki halali wa kiwanja hicho.
Amesema vurugu hizo ambazo zimesimamisha shughuli zote biashara na kukwamisha pia usafiri katika barabara kuu ya Tunduma, zilianza siku ya jumatatu baada ya wananchi kuhamasishwa na kuvamia uwanja huo na kuanza shughuli za ujenzi wa Zahanati pamoja na Kituo cha polisi, ambapo polisi waliingilia kati na kuwazuia.
Kamanda Msangi amesema watu 26 walikamatwa siku ya Jumatatu katika vurugu hizo ambazo zilisambaa katika barabara kuu na kusababisha barabara kufungwa kwa kuwekwa mawe ambapo pia gari moja la polisi lilivunjwa vioo
Amesema baada ya jana hali kutulia kidogo leo tena vurugu hizo ziliibuka baada ya wananchi kukutana na mbunge wa eneo hilo kupitia Chadema Mhe. David Silinde ambapo wananchi walirejea tena kufanya vurugu mitaani na kufunga barabara kwa mawe na kuchomamoto matairi ya gari, hata hivyo polisi walituliza hali hiyo.

Related Posts:

  • January Makmba kufunguka jumapilu ijayo   Mbunge wa Bumbuli, Tanga na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba nae ni mmoja wa walioingia kwenye headlines kwamba na yeye ameingia kwenye list ya wagombea wa CCM kwenye nafasi ya U… Read More
  • Waziri:Mbeki ndiye aliyetoa fedha kwa FIFA    Thabo Mbeki Waziri wa michezo wa Afrika Kusini , Fikile Mbalula, sasa anasema rais wa zamani wa Afrika kusini Thabo Mbeki ndie aliyeruhusu ulipwaji wa fedha ,dola milioni 10 kwa FIFA , hela ambayo sasa i… Read More
  • Mbiyo za Urais ndani ya CCM, Mwigulu Nchemba achukua fomu leo      Mbio za kumpata mlithi wa kiti cha urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, zinazidi kushika kasi ndani ya chama cha mapinduzi-CCM baada ya wanachama kuzidi kuongezeka katika harakati za kumpata mgombe… Read More
  • Mwasiti amshtua Babu Tale Ukimya wa msanii wa Bongo Fleva,Mwasiti Almas kwenye muziki umemshtua meneja wa msanii Diamond,Babu Tale. Babu Tale alimzungumzia msanii huyo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha XXL ambapo a… Read More
  • Kituo cha tembo yatima chafunguliwa   Srikali ya Tanzania imeanzisha kituo cha kwanza cha tembo yatima mjini Arusha. Kituo hicho kinatarajiwa kuhifadhi watoto wa tembo waliopoteza wazazi wao kutokana na vitendo vya ujangili au sababu nyengine. Hatua … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE