Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba,Posta jijini Dar.
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea gari na kumuovateki na kuligonga gari lake. Aidha alisema kuwa alisikia maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata majeraha kwa ndani. ‘’Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na wasiwasi labda niliumia kwa ndani,’alisema Keisha.
MRADI WA TAZA MBIONI KUKAMILIKA - KAPINGA
-
📌 Unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Iringa hadi
Sumbawanga
📌 Kapinga asema Mkoa wa Rukwa kuunganishwa na gridi ya Taifa kupitia mrad...
32 minutes ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment