Takriban watoto 80 waliookolewa katika kambi ya kundi la Boko Haram nchini Cameroon hawawezi kukumbuka majina yao kulingana na afisa mmoja aliyewatembelea. Watoto hao wenye umri wa miaka 5 hadi 18 hawakuzungumza kiingereza,kifaransa ama lugha nyengine yeyote ile kulingana na Christopher Fomunyoh,ambaye ni mkurugenzi wa kitaifa wa taasisi ya National Democratic Institute {NDI}. Watoto hao walipatikana katika kambi kazkazini mwa Cameroon mnamo mwezi Novemba. Kundi la Boko Haram kutoka Nigeria limepanua mashambulizi yake hadi nchini Cameroon. Wapiganaji hao wanajaribu kusimamisha taifa lenye uongozi wa kiislamu kazkazini mashariki mwa Nigeria. Wanadhibiti miji kadhaa na vijiji katika jimbo hilo na hivi majuzi waliahidi kuiga mfano wa kundi la Islamic State ambalo limeteka eneo kubwa la Syria na Iraq
TAWA YAKABIDHI BWENI LA WASICHANA SHULE YA SEKONDARI MCHENGERWA, RUFIJI
-
Na Beatus Maganja, Rufiji, Pwani.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imekabidhi rasmi bweni
jipya la wasichana katika Shule ya Sekondari...
3 hours ago





0 MAONI YAKO:
Post a Comment