.jpg)
Rais Kikwete akiingia uwanjani
Rais Jakaya Kikwete wa Jamhuri ya Muungano wa leo amwaongoza Watanzania
katika kuadhimisha miaka 51 ya kuzaliwa kwa Tanzania baada ya
kuunganisha nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
.jpg)
Muungano huu
umeasisiwa na mashujaa wa nchi hii ambao ni Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume tarehe 26/4/1964. Muungano ulifanyika baada ya nchi hizi mbili kujipatia uhuru wake ambapo
Tanganyika ilipata uhuru mwaka Desemba 1961 na Zanzibar Januari 1964.
.jpg)
Rais Kikwete akikagua gwaride la heshima katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Katika sherehe hizo Watanzania watashuhudia matukio kadhaa yakiwemo ya
kijeshi ambapo gwaride lililioandaliwa na vikosi mbalimbali vya ulinzi
na usalama litapita kwa mwendo wa taratibu na mwendo wa kasi pamoja na
ndege za kivika kupita huku zikionesha manjonjo yake katika kutoa
heshima kwa rais Kikwete Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi na Usalama. Mbali na hayo pia kutakuwa na halaiki ya
watoto wakionesha mambo mbalimbali yanayohusiana na sherehe hii ya leo.
Ndani ya miaka hiyo 51 mataifa hayo yamepiga hatua katika maendeleo
makubwa tofauti na wakati zinaungana. Maadhimisho ya mwaka huu
yatapambwa na Kauli Mbiu isemayo Miaka 51 ya Muungano, Tudumishe Amani
Na Umoja, Ipigie Kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa na Kushiriki
Uchaguzi Mkuu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment