May 17, 2015

Prof-Jay 
Ikiwa imebaki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika kwa Tanzania,staa wa muziki wa Bongo Fleva ambaye amedumu kwa zaidi ya miaka 15 mtu mzima Profesa Jay anayo ya kusema na Rais Jakaya Kikwete.
Profesa Jay kwenye Exclusive na Amplifaya ametoa sentensi 3 ambazo kama akikutana na Rais leo angemwambia,sentensi ya kwanza amesema kuwa angemwambia Rais awe na maamuzi magumu kwa sababu kama tunachukia Rushwa na ufisadi basi na yeye awe mkali,atumie madaraka aliyonayo kwa sababu anaamini ana uwezo wa kuirudisha Tanzania kwenye mstari.
Sentensi yake ya pili  amesema angemwambia asicheke na Nyani kwani ndio maana anaona tunavuna mabua na huku akimsifia kwa kumwambia mheshimiwa unafanya kazi yako vizuri lakini wanaokuangusha ni watu waliokuzunguka.
Sentensi ya tatu ya Profesa Jay kwenda kwa Rais Kikwete amesema angemwambia Rais awe mkali zaidi atumie nafasi yake kama Rais ili Rushwa na Ufisadi vimalizike ili tuweze kuona matunda ya Tanzania.
 Hii imetokaktaika website pendwa Tanzania ya Millardayo.com

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE