Polisi wawili wameuawa katika machafuko yanayoendelea nchini Burundi
katika mwendelezo wa maandamano ya wapinzani ya kupinga hatua ya Rais wa
nchi hiyo Pierre Nkurunziza ya kuamua kugombea katika uchaguzi mkuu
ujao nchini humo. Polisi ya Burundi imetangaza kuwa, mbali na polisi hao
wawili, mtu mmoja mwengine alipoteza maisha katika shambulio hilo
lililotokea jana usiku jijini Bujumbura. Kwa mujibu wa mashuhuda,
shambulio hilo lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku katika eneo la
Kamenge, kaskazini mashariki mwa mji huo. Maandamano ya kupinga uamuzi
wa Rais Nkurunziza kutaka kugombea katika uchaguzi wa rais ujao,
yamezorotesha uchumi wa nchi hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo rais
huyo ameendelea kushikilia msimamo wake wa kugombea kwenye uchaguzi
huo. Akihutubia sherehe za Mei Mosi hapo jana, Rais huyo kijana, mbali
na kukosoa maandamano ya wapinzani aliwataja watu wanaoandamana kuwa ni
watoto wadogo wanaojiingiza katika mambo yasiyowahusu.
MTEMI MAKWAIA WA III AHIMIZA UPENDO KUWA NI NGUZO YA MAENDELEO BUSIYA
-
Chifu wa Utemi wa Busiya Faustine Makwaia wa III akizungumza kwenye sherehe
za Tamasha la utamaduni la Sanjo ya Busiya katika viwanja vya Ikulu ya
utemi h...
1 hour ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment