Staa wa Bongo Fleva anaye fanya vizuri kwa sasa na ngoma yake ya
‘Sophia’ Ben Pol amefunguka kuwa atafunga ndoa ya kimila kwenye harusi
yake.
Akipiga stori na Clouds Fm hivi karibuni,alisema kuwa atafunga ndoa
ya kimila ya kabila lake la Kigogo atakapofunga ndoa na mchumba wake
aliyedumu naye kwa muda mrefu.
‘’Napenda sana mila hasa za kabila letu la Kigogo ndiyo maana mipango
yangu ni kufunga ndoa ya kimila na kila kitu kitakuwa cha kimila
kuanzia mavazi,keki na chakula,’’alisema Ben Pol
0 MAONI YAKO:
Post a Comment