Shirika la maafisa wa polisi wa
kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita
wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.
Agizo
hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa
wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo
aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.
Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.
Ilani
hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili
wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe
,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment