June 05, 2015

mwasiti

Ukimya wa msanii wa Bongo Fleva,Mwasiti Almas kwenye muziki umemshtua meneja wa msanii Diamond,Babu Tale.
babu tale
Babu Tale alimzungumzia msanii huyo hivi karibuni alipokuwa akifanya mahojiano kwenye kipindi cha XXL ambapo alisema kuwa kukaa muda mrefu bila kutoa ngoma hawatendei haki mashabiki wake.
mwasiti2 
‘Mwasiti ni msanii mzuri sana na pia ni balozi lakini anapokaa muda mrefu bila kutoa ngoma anakuwa hawatendei haki mashabiki wake,’alisema Babu Tale.
Akijibu sababu ya kuwa kimya Mwasiti alisema kuwa ukimya wake alikuwa akifanya mambo mengine nje ya muziki lakini anatarajia kuachia ngoma mapya mwezi huu ulitwao Sema Nawe ambao ameufanya katika studio za Swich Records chini ya producer Lufa.
‘’Nategemea kuwapa zawadi mashabiki wangu mwezi huu nitaachia ngoma yangu mpya,na pia namshukuru sana Babu Tale kwa kunipa moyo kwani huwa ananisema kila wakati nitoe ngoma,’alisema Mwasiti.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE