SHIRIKISHO la soka TanzaniaTFF
limezitaka klabu kushirikiana na SPUTANZA pamoja na Bodi ya Ligi katika
kuweka mifumo mizuri ya uingiaji mikataba.
TFF inao mkataba mama (template) ambao klabu zote na wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual contracts between players and clubs).
Hayo yamekuja baada ya kuibuka kwa utata wa mkataba wa Ramadhan Singano ‘Messi’ na klabu yake ya Simba.
Singano alikuwa na mkataba wa
miaka miwili unaoisha mwezi Julai mwaka huu 2015, wakati Simba wao
walikuwa na mkataba wa miaka mitatu utakaoisha mwezi Julai mwakani.
Katika kikao cha jana ambapo TFF
iliwakutanisha Singano na Simba, pande zote zilieleza kutambua utata
ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya
uongozi wa sasa wa Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo mbili
zimekubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba
mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
Kutokana na maamuzi hayo, Singano
ametoa kauli hii: “Wamesema tukae chini tuongee, mikataba yote haipo,
kisheria mimi niko huru” “Tukishindwa kukubaliana inabidi nitafute timu
nyingine, lakini kipau mbele ni kuongea nao (Simba) kama kweli wana nia
au hawana nia na mimi”.
Hata hivyo Singano alitamka bayana kuwa hawezi kuelewana tena na Simba na hii inaashiria safari ya kutua Azam fc inanukia.
Azam fc wana mpango wa kumsajili Singano endapo utata wa mkataba wake utamalizika na walishaeleza wazi kuiwania saini yake.
Kikubwa inabidi nipewa mkataba
niangalie na kuweka vitu vyangu. Niwashauri wachezaji wenzangu, bora
ukose vitu vyote kuliko kukosa mtu wa kukuongoza, ukikwama utasaidiwa
0 MAONI YAKO:
Post a Comment