July 17, 2015

banza (1)
Muimbaji wa Twanga Pepeta, Banza Stone afariki dunia
Muimbaji wa muziki wa dansi nchini Banza Stone amefariki dunia Ijumaa hii baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Banza alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Banza ambaye jina lake halisi ni Ramadhan Masanja alikuwa akisumbuliwa na maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kichwa.
Msiba wake upo nyumbani kwao maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam. Wasanii mbalimbali wametumia mitandao ya kijamii kutuma salamu za rambi rambi kufuatia msiba huo.
Banza Stone alisifika kwa uwezo wake mkubwa wa utunzi wa nyimbo na uimbaji na amewahi kufanya kazi na bendi mbalimbali nchini zikiwemo TOT na Twanga Pepeta.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE