Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje nchini, Bernard Membe, amesema
hatogombea wadhifa wowote kwenye uchaguzi mkuu ujao na
kwamba anapanga kujishughulisha na masuala yake ya kibinafsi.
Membe ambaye alikuwa akitafuta tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kuwania urais mwezi Oktoba lakini akashindwa kufikia lengo hilo, amesema kuwa, hatotafuta nafasi ya ubunge katika jimbo lake la Mtama. Hata hivyo amesema ataendelea kukiunga mkono chama chake cha CCM na atampigia debe mgombea urais aliyeteuliwa na chama hicho, Bw. John Magufuli.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba Membe angegombea ubunge baada ya kukosa nafasi ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM.
Huku hayo yakijiri, chama tawala nchini CCM kinaendelea kupata pigo baada ya baadhi ya wabunge wake kutangaza kuwa hawatogombea tena nafasi zao kupitia chama hicho kwenye uchaguzi mkuu ujao. Mbunge wa Kahama, James Lembeli ni mwanachama wa CCM wa hivi karibuni kutangaza kuwa hatatetea kiti chake kupitia chama hicho kwenye uchaguzi wa Oktoba mwaka huu. Tayari madiwani 20 wa CCM katika jimbo la Monduli wametangaza kuhamia Chadema na kumtaka mbunge wao, Edward Lowassa kufuata mkondo huo.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment