July 16, 2015


Jana akiwa nyumbani kwake Mwanasiasa Mgongwe nchini na Muasisi wa Chama cha Mapinduzi – CCM, Mzee Kingunge Ngombari Mwiru aliongea na waandishi wa habari na kutoa maoni yake juu ya mchakato mzima wa chama chake cha Mapinduzi kilivyompitisha mgombea wao atakayewakilisha chama nafasi ya Urais hapo oktoba 25, ambaye ni Dk. John Pombe Magufuli.
Mzee Kingunge alisema wazi kwamba akuridhishwa na mchakato mzima ulivyokwenda na kulaumu kamati nzima iliyofanya maamuzi hayo.
“Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katok kuwajadili wagombea, lakini safari hii kamati imefanya kazi isiyowahusu kikatiba – kukata majina ya wagombe”, alisema Mzee Kingunge.
Mzee huyo alisema kwamba Kamati ya maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama na wala haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38.
Pia Mzee, Kingunge alionyesha wazi chaguo lake kuwa ni Mh. Edward Lowassa kwani tangu mwanzo alionyesha kupendwa na watu.
Lakini licha ya Lawama zote hizo Mzee Kingunge alisema ataendelea kuwa mwanachama muadilifu ndani ya chama hicho.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE