Miss
Tanzania 2006,Wema Sepetu alipokuwa akijiandaa kulipa ada ya uchukuzi
wa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa Singida leo
(17/7/2015).Kulia ni katibu UWT wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu, akitoka ndani ya ofisi ya CCM wilaya ya
Ikungi baada ya kukabidhiwa fomu za kuwania ubunge viti maalum mkoa wa
Singida.Nyuma ni mama yake, Mariamu Sepetu.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Ikungi
MSANII
wa filamu maarufu nchini Wema Isaac Abraham Sepetu,amechukua fomu ya
kuomba kugombea nafasi ya viti maalimu CCM mkoa wa Singida na kuahidi
kwamba lengo lake ni kuja kushirikiana na wanawake na wakazi kwa ujumla
kuuletea maendeleo zaidi mkoa huo.
Wema
ambaye amewahi kuwa miss Tanzania 2006,ameahidi kutumia nguvu zake zote
na uzoefu wake katika kutumikia jamii,kusaidiana na wanawake katika
kujiletea maendeleo yakiwemo na ya uchumi.
Alisema
kwa muda mrefu amekuwa akiisaidia jamii ya jijini Dar-es-salaam na sasa
ameamua kwa dhati kuelekeza nguvu zake katika kuitumikia jamii ya
nyumbani kwao mkoa wa Singida.
“Pia
natarajia kukaa chini na vijana wa mkoa wangu wa Singida,ili kwanza
nijue chanagamoto zinazowakabili halafu kwa pamoja,tuweke mipango na
mikakati ya namna ya kuzipatia ufumbuzi wa kudumu changamoto hizo”,
alisema.
Wema
alisema kuwa ni nitaelekeza nguvu zangu kwa wanawake wenzangu…..nisikie
vilio vyao ili iweze kupata mwelekeo wa namna ya kuwasaidia waweze
kujiendeleza kwa manufaa ya familia zao,mkoa na taifa kwa ujumla.
Kuhusu
sekta ya usanii,alisema endapo CCM kitampitisha na kufanikiwa kuwa
mbunge wa viti maalum,atatumia fursa ya kuwa kiongozi mwenye uwezo wa
kuwasaidia wasanii mbalimbali pamoja na mambo mengine,wasiibiwe kazi
zao.
“Kwa
kweli niwahakikishie wasanii wenzangu kuwa nikifanikiwa kuwa
kiongozi,nitahakikisha kazi zao haziibiwi tena na pia kuwepo kwa
mazingira rafiki yatakayo wasaidia kufanya kazi zao bila vikwazo vyo
vyote”,alisema Wema.
Chanzo: Moe Blog
0 MAONI YAKO:
Post a Comment