August 24, 2015



Wakali wa London, timu ya Arsenal imekubali kutoka sare ya bila kufungana na timu ya Liverpool katika mchezo wa Premier League uliochezwa uwanja wa Emirates usiku wa jana .
Shukrani kwa mlinda mlango wa Gunners, Petr Cech aliyecheza kwa kiwango cha hali ya juu kwa kuzuia michimo miwili ya  wazi iliyokuwa inaelekea langoni kwake ya mshambuliaji mpya wa Liverpool , Christian Benteke na mpira wa kiungo Philippe Coutinho kipindi cha kwanza.
Mchezaji Aaron Ramsey aliweza kukwamisha  mpira kambani lakini mwamuzi wa mchezo huo alikataa, mchezaji huyo alikuwa amekwisha kuotea,
Kila timu ilionyesha makali yake huku ikishuhudiwa timu ya Liverpool wakitawala kipindi cha kwanza cha mchezo huo,  huku Arsenal wakirudi baada ya kutoka mapumziko na kumiliki mpira na kudhibiti mchezo huo uliokuwa na upinzani. Arsenal imefikisha pointi nne katika michezo mitatu waliyocheza huku Liverpool ikikusanya pointi 7 katika michezo mitatu ya Premier League.Kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho amekuwa mchezaji bora wa mechi hiyo ya usiku.
kikosi cha Arsenal kilichoanza mchezo wa jana ni, Cech, Bellerin, Chambers, Monreal, Coquelin, (Oxalde-Chamberlain 82), Ramsey, Ozil,Cazorla, Sanchez, Giroud, (Walcott 73)
Huku Liverpool ikiwakilishwa na Mignolet, Clyne, Lovren, Skrtel, Gomez, Can, Milner, Lucas, (Rossiter 76), Coutinho, (Moreno 88), Firmino (Ibe 63) Benteke.




Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE