August 27, 2015

.

Kutoka katika chumba cha habari cha TZ kilichopo Ubungo Tanznaia, tunapata habari hii inayohusu kuundwa kwa kamati mpya ya Miss Tanzania
Shindano la kumsaka mrembo Miss Tanzania limerudi rasmi, na leo kulifanyika utambulisho wa kamati mpya itakayohusika kusimamia tamasha hilo.
Kwa mujibu wa msemaji wa kamati hiyo mpya, Jokate Mwegelo..‘Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu ns kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.
.
Picha ni wajumbe wa kamati mpya ya Miss Tanzania, Jokate na Juma Pinto (Katikati Mwenyekiti wa kamati hiyo).
‘Tumekubali na tumepokea majukumu hayo na kuahidi kusimamia kanuni, Sheria na Taratibu za kuendesha mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.Tunaomba jamii ya Watanzania watupe ushirikiano pamoja na kutuamini kwamba tunaweza kuisogeza mbele zaidi tasnia hii ya urembo hapa nchini’ – Jokate Mwegelo
‘Kwa leo hatutakuwa na mengi ya kusema kwa sababu ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili hivyo kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka yetu  ya Tanzania’ – Jokate Mwegelo
3X6A5818
Wajumbe wa kamati mpya ya Miss Tanzania, Jokate Mwegelo na Juma Pinto ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.
3X6A5832
Waandishi wa Habari.
.
Miss Tanzania 2014, Lilian Kamazima.
Kamati Mpya ya Miss Tanzania inaundwa na wajumbe wafuatao
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Kwa upande wa Sekretariet tunao wajumbe 4 ambao ni
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

Habari na picha ni kutoka chumba cha Habrai chaTZA

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE