Mjumbe wa shina namba 20 wa mtaa wa ulongoni a, kata ya gongo lamboto jijini Dar es Salaam, amekamatwa baada ya kukutwa akiandikisha majina na namba za vitambulisho vya kupigia kura.
Mjumbe huyo wa CCM anayefaahmika kwa jina la Mustapher Juma ametiwa nguvuni baada ya kuendesha zoezi la kuandika majina na namba za vitambulisho vya kupigia kura huku akiwalaghai wenye vitambulisho hivyo kuwa watakuwa wanufaika wa kwanza pindi taasisi ya fedha ya umoja Saccos itakapoa anza kufanya kazi zake.
Katika mahojinao yake na ITV mjumbe huyo wa shina namba 20 wa mtaa wa Ulongoni A, amekiri kupatia fomu maalum ya kuandika majina na namba za vitambulisho vya kupigia kura huku akisisitiza kuwa alipewa kazi hiyo na moja ya viongozi wake wa tawi bila kujua matumizi ya namba hizo.
Chanzo cha habari hii kilipojaribu kumtafuta Bw Thomas Mwita Kimbaru anayedaiwa kumpatia fomu hiyo mjumbe huyo wa shina, alisema hahusiki na chochote na kwamba si msemaji wa chama, katika hatua nyingine mtandao wa asasi za kiraia za kutazama uchaguzi nchini umeonyesha kutokurishwa na vitendo mbalimabli vilivyoanza kujitokeza katika zoezi la kampeni hasa matumizi ya lugha za matusi huku wakiitaka tume kuhakikisha inasimamia sheria.
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi kwa sasa maandalizi yote ya uchaguzi yako vizuri huku ikiendelea kusisitiza vyama kuhakikisha vinatii na kuheshimu misingi ya siasa safi na kutokuwa chanzo cha kufanya uchaguzi kutokuwa huru na haki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment