Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imesema kuwa, maafisa 110 wa vikosi
vya ulinzi wamefutwa kazi kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na magenge ya
kigaidi.
Msemaji wa wizara hiyo amesema kuwa, maafisa hao ni kutoka vikosi mbalimbali vya polisi, gadi ya taifa, jeshi na maafisa wa forodha.
Louguini ameongeza kuwa, maafisa hao wanakabiliwa na tuhuma kali sana za kuwa wanachama wa magenge ya kigaidi au kushirikiana nao.
Amesema hatua hizo za lazima zimechukuliwa baada ya kufanyika uchunguzi wa kina tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Tarehe 24 Julai, bunge la Tunisia lilipitisha sheria mpya ya ugaidi kama juhudi za kupambana na wimbi hilo katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Sheria hiyo imetoa mamlaka ya kutolewa adhabu ya kifo kwa makosa kadhaa ya ugaidi, ijapokuwa nchi hiyo haijawahi kutekeleza adhabu ya kifo tangu mwaka 1991. Sheria hiyo inaruhusu pia kuwekwa kizuizini watuhumiwa wa ugaidi kwa muda wa siku 15 bila ya kukutana na mawakili.
Taarifa zinasema kuwa, idadi kubwa ya wanachama wa genge la kigaidi la Daesh ni kutoka Tunisia na Morocco

0 MAONI YAKO:
Post a Comment