September 23, 2015

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ACT Wazalendo Khamis Iddi Lilla amewahakikshia wazanzibari kuwa serikali yake itapambana na waletaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya kwa kuunda kikosi maalum cha kisasa cha kupambana na vita hivyo.
Mgombea huyo wa ACT Wazalendo Khamis Iddi Lilla ametoa ahadi hiyo alipokuwa akinadi sera katika viwanja vya Kiembesamaki ambapo amesema chama cha ACT kinawajua waletaji hao wa madawa ya kulevya na serikali yake itaunda kikosi cha kisasa chenye vitendea kazi vyote vianavyohitajika.
 
Akizungumzia utendaji wa serikali katika kushugulikia sekta za kijamii mgombea huyo amesema kazi ya kwanza akiingia madarakani itakuwa ni suala la kutoa elimu kwa watoto hadi wazee na afya hospitali na vituo vyote kuwa na madawa na madaktari.
 
Naye mgombea mwenza wa rais wa muungano wa ACT Wazalendo Hamad Mussa akitafuta kura aliwataka wazanzibari wabadilike na kuacha kukumbatia vyama vya CCM na CUF.
 
Kutokana na siku kuu ya Iddi el haj karibu vyama vyote vimesimamisha kampeni zao hadi kuanzia jumatatu ambapo chama cha NRA kitafanya mkutano wake wa kwanza huku CCM, CUF, ACT Wazalendo na ADC na vyama vyingine vikiendelea na kusaka urais wa Zanzibar.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE