September 14, 2015

Akihojiwa na mtangazaji Tido Mhando katika kipindi cha mikikimikiki AZAM 2 TV leo asubuhi, Zitto ameshangazwa na hatua ya mgombea urais kupitia CCM kujipambanua kuuchukiaufisadi wakati kipindi chote cha mijadala ya ufisadi wa EPA, MEREMETA, BUZWAGI, TOKOMEZA, RICHMOND, ESCROW nk hakuwahi kukemea lolote.

ZITTO alienda mbali zaidi kuhusiana na kauli ya Magufuli hivi karibuni akiwa Tanga kwamba atayarejesha mashamba ya mkonge kwa wananchi ilihali yeye Zitto alileta hoja hiyo ya mkonge bungeni na Magufuli aliungana na wenzie kuipinga hoja hiyo kwa macho makavu, leo anaudanganya umma kuwa atayarejesha ni usanii mkubwa.

Amewaomba Watanzania kumchagua mama ANNA MGWIRA maana ndiye pekee asiye na makandokando tofauti na wagombea wengine!!

Chanzo: AZAM II TV

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE