.Wanamuziki
Ben Paul na Fid Q wanaoshiriki kwenye onyesho la Coke Studio wakiwa
katika picha ya pamoja na washabiki wao wakati wa uzinduzi wa onyesho
hili jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Sehemu ya wafanyakazi wa kiwanda cha Coca Cola Kwanza wakifuatilia onyesho la Coke Studio.
Msimu
wa Coke Studio umewahusisha pia wanafunzi mashuleni kuonyesha vipaji
vyao kama anavyoonekana mwanafunzi akionyesha kipaji cha kucheza katika
moja ya tamasha la Coke Studio lililofanyika mjini Mwanza hivi karibuni.
Mwanamuziki nguli wa Bongo
Fleva nchini Ben Paul amesema kuwa ushiriki wake katika onyesho la Coke
Studio ni moja ya mafanikio katika safari yake ya muziki.
Katika mahojiano aliyoyafanya
wiki hii kuhusiana na ushiriki wake katika onyesho hili maarufu
linaloendeshwa na kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha kolabo za
wanamuziki mbalimbali wa Tanzania na nje ya nchi alisema anajivunia
ushiriki wake katika onyesho hili na ameweza kujifunza mengi kuhusiana
na fani ya muziki.
“Japo hapo awali nimewahi
kushinda tuzo mbalimbali za muziki lakini ushiriki wangu katika onyesho
hili kubwa la kimataifa ni moja ya mafanikio yangu makubwa katika
safari yangu ya muziki.
Alisema anajisikia fahari
kufanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki Wangechi kutoka nchini
Kenya katika msimu huu wa Coke Studio ambapo kwa hapa nchini onyesho
hilo linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia
luninga ya Clouds.
Ben Paul alisema onyesho la
Coke Studio linahamasisha vijana kujiamini na kuonyesha vipaji vyao na
aliwataka vijana wenzake kujiamini na kutokata tamaa iwapo wanataka
kutimiza ndoto zao na kufanikiwa katika maisha.
Alisema katika safari yake ya
muziki amekutana na changamoto nyingi mojawapo ikiwa ni kunyimwa nafasi
ya kurekodi nyimbo zake na waandaaji mbalimbali wakiamini kuwa hakuwa na
uwezo wa kuimba lakini licha ya kufanyiwa hivyo aliendelea kupambana
mpaka kufanikiwa kufika alipo sasa.
“Ninachotaka kuwaambia ni
kwamba, mfano, kwa wale wenye vipaji vya kuimba, kitu kikubwa
unachotakiwa kufanya ni kuwa na nyimbo nyingi ambazo, hata ukirekodi
moja isipofanya vizuri, unatoa nyingine ili kuhakikisha unaendelea
kusikika masikioni kwa watu”, alisema
Aliwaasa vijana wa jinsia zote
kujiamini na kuondokana na dhana kwamba jinsia fulani ndio wanaweza
kufanya kitu fulani na kusisitiza kuwa kila mtu ana kipaji na anaweza
kufanya mambo makubwa.
Alimalizia kwa kuwapongeza
wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu huu wa
tatu wa Coke Studio mwaka huu. Wanamuziki hao ni Fid Q ambaye amefanya
kolabo (mash-up) na Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo
(mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka Nigeria na Ali Kiba ambaye
amefanya Kolabo na mwanamuziki Victoria Kimani.
Lengo kuu la Coke Studio Afrika
ni kuwakutanisha kwa pamoja wasanii wenye mbalimbali wa Afrika na
kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko.
Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na
wasanii wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao
na kuzidi kukuza vipaji vyao
Onyesho la Coke Studio
linarushwa kila siku ya Jumamosi saa kumi na mbili jioni kupitia luninga
ya Clouds. Pia unaweza kusikiliza kipindi cha Coke Studio kwenye Clouds
FM kila Jumamosi saa nne asubuhi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment