November 07, 2015

Ni siku moja baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa kiti cha Urais ameanza kazi yake kwa surprise, Rais JPM amekatisha kwa mguu kutoka Ikulu mpaka Wizara wa Fedha maeneo ya Posta na kukuta ndani ya Ofisi kuna wafanyakazi ambao hawapo Ofisini na ilikuwa ni muda wa kazi.

ripota wa millardayo.com alikutana na shuhuda akielezea namna alivyotembelea kutoka Ikulu mpaka kuingia Wizara ya fedha..’Mimi niliona watu walikuwa wanakimbia kumbe alikuwa ni rais wa awamo ya tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli  anatembea kutokea Ikulu akielekea Wizara ya Fedha au hazina alikuwa na walinzi pamoja na magari yake yalikuwa yakitembelea’ – Shuhuda

‘Baada ya kutoka wizara ya fedha basi akaingia kwenye  gari, mimi hii ni mara yangu ya kwanza kuona kiongozi kama huyu ameapishwa jana na leo ameanza kufanya kazi basi atakuwa kweli ni Rais wa tofauti kabisa’ – Shuhuda
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Shuhuda akieleza jinsi Rais JPM alivyoingia wizara ya Fedha

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE