Mwanafunzi
wa mwaka 3 wa Chuo cha CBE Bw. Wilson Magembe anayesomea Utawala wa
BIashara akitoa ufafanuzi kwa wageni mbalimbali waliotembelea banda la
Maonesho la Utawala wakiongozwa na Mkuu wa Chuo hicho Prof. Emanuel
Mjema (kulia)wakati wa hafla ya Utoaji wa Tuzo na Zawadi mbalimbali kwa
wahitimu wa chuo hicho mwaka 2015.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
[DAR ES SALAAM] Taasisi
za elimu kote nchini zimeaswa kujenga utamaduni wa kuthamini na
kutambua mchango wa wahitimu wanaofanya vizuri katika masomo yao
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya
Biashara Dar es Salaam (CBE) Prof.Emanuel Mjema wakati wa hafla ya
kuwatunuku vyeti na zawadi mbalimbali wahitimu wa chuo hicho takribani
20 waliofanya vizuri katika masomo yao kwa mwaka 2015.
Akizungumza
na jamii ya wanachuo na Wahitimu wa Zamani wa Chuo cha Elimu ya
Biashara na wale wanaofanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini amesema
chuo chake kina utamaduni wa kuwatuza wahitimu wanaofanya vizuri katika
masomo yao kama motisha kuthamini juhudi zao ili kuhamasisha wengine
kufanya vizuri zaidi.
Amesema
wahitimu 20 wa fani mbalimbali zikiwemo za Rasilimali Watu,Uendeshaji
wa Biashara, Ununuzi na Ugavi, Vipimo na Mizani, Uhasibu, Ununuzi na
Ugavi, Masoko na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ngazi ya
Stashahada, Shahada,Diploma na Cheti wametunukiwa vyeti na kukabidhiwa
zawadi mbalimbali.
Mmoja wa Wahitimu wa CBE
aliyefanya vizuri katika fani ya Rasilimali Watu Bi. Happyness Onani
akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Prof.Emmanuel Mjema.
Prof.
Mjema ameongeza kuwa mbali na tuzo hizo wadau hao hususan wahitimu wa
miaka ya nyuma wa chuo hicho wapata fursa ya kujadili masuala mbalimbali
ikiwemo kukijengea uwezo chuo hicho pamoja na kuangalia shughuli za
kitaaluma zinazofanyika.
”
Siku hii ni muhimu sana kwa Chuo cha Elimu ya Biashara, ni siku ambayo
tunathamini wahitimu wetu waliofanya vizuri kwa kuwapa Zawadi za vtu
mbalimbali kuthamini mchango na heshima waliokipa chuo chuo chetu”
Alisisitiza Prof.Mjema.
Ameongeza
kuwa utoaji wa zawadi na tuzo hizo unakwenda sambamba na na maadhimisho
ya ya Mahafali ya 50 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam
yatakayofanyika Novemba 12,2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo
mgeni rasmi atakua Rais mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hasani Mwinyi.
Baadhi ya wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Zawadi na kwa wahitimu iliyofanyika CBE kampasi ya Dar es Salaam.
Akifafanua
kuhusu mahafali hayo ya 50 amesema kuwa wahitimu wapatao 2050 wa ngazi
mbalimbali watatunukiwa Shahada , Astashahada, Stashahada, shahada na
stashahada za Uzamili.
Kuhusu
suala la nidhamu chuoni hapo hasa mavazi amesema kuwa chuo chake
kimeendelea kusisitiza nidhamu na kuweka kanuni zinazowabana wanafunzi
huku akifafanua kuwa chuo hicho kilikua chuo cha kwanza kuweka sheria
inayosimamia nidhamu ya mavazi kwa wanafunzi.
Amesisitiza
kuwa mavazi ndiyo yanayompambanua mwananfunzi na kuonyesha tabia yake
na kuongeza kuwa nidhamu inapokua juu inawapa wanafunzi fursa nzuri ya
kupata ajira pindi wanapohitimu kwa kuwa tayari wanaaminika katika
jamii.
Wageni
mbalimbali wakitembelea eneo la Vipimo na Mizani wakati wa hafla
ya utoaji wa Tuzo na zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo
yao katika Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam.
Prof.Mjema
amebainisha hali ya nidhamu ya mavazi inaendelea kuzingatiwa kutokana
na Madhara ya kuzuiwanna kushindwa kuhudhuria vipindi wanayoyapata
wanafunzi waliokuwa wanakiuka kanuni na taratibu za chuo hicho
“Vijana
lazima wawe mfano wa kuiga na hawa ni wasomi ambao wanategemewa na
taifa, CBE imeshafukuza wengi kwa kukosa nidhamu, pia mwanafunzi
anayekosa maadili huathiri maendeleo ya chuo na wanafunzi wengine”
Amesisitiza.
Akizungumza
kwa niaba ya wahitimu wa zamani wa chuo hicho (Alumnae) Bw.Lusekelo
Mwandemange amesema kuwa wao kama wahitimu wanayo dhamana ya
kuhakikisha maendeleo ya chuo hicho yanapatikana.
Amesema
wahitimu hao wamekuwa kioo kwa jamii inayowazunguka kwa kuitumia elimu
yao kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii
Aidha
wameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kuendelea kuweka mazingira
rafiki ya kuwawezesha wanafunzi wa chuo hicho katika fani mbalimbali
kupata elimu yenye viwango ndani na nje ya nchi.
Pia wamesema kuwa wao kama wahitimu wameanzisha umoja wao utakaohusika kuchangia maendeleo ya chuo hicho
Bw. James Mkuwa –
Muhadhiri Msaidizi Idara ya uongozi wa Biashara CBE akitoa ufafanuzi kwa
wageni mbalimbali kuhusu elimu ya Biashara wanayoitoa
kwa wajasiriliamali ,wanafunzi ngazi ya shahada na cheti pia wale
wanaotaka kufungua kampuni na BIashara kwa kuwapatia taaluma ili
wajiandae kujiajili wenyewe.
Kutoka:dewjiblog.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment