Mourinho alikuwa tayari amekiri Chelsea hawawezi kumaliza katika nne bora ligini
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya.
The
Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo
yamekuwa kinyume, na wamo nafasi moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja
ligini.Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich.
- Bodi ya Chelsea yamjadili Mourinho
- Guardiola kuweka wazi hatima
- Mourinho: Naona aibu
Chelsea walimaliza alama nane mbele kileleni msimu uliopita na kutwaa taji pamoja na Kombe la Ligi lakini mwaka huu wameanza vibaya, wakishindwa mechi tisa kati ya 16 ligini kufikia sasa.
mechi ya mwisho kwa Mourinho kwenye usukani ilikuwa Jumatatu walipochapwa na viongozi wa ligi Leicester City 2-1.
Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos na miongoni mwa wanaopigiwa upatu kumrithi
Kwa hisani ya BBC
0 MAONI YAKO:
Post a Comment